Tuesday, March 26, 2019

JE? WAJUA: HOTELI YA KWANZA ANGA ZA JUU



Duniani tumezoea utalii ufanywa tuu chini ya ardhi ya dunia, je?  umewahi kufikiria kuwepo kwa utalii wa anga za juu mfano, utalii katika mwezi au katika sayari angani, basi utakubaliana na mimi kuwa hii ni aina mpya ya utalii. Mwaka jana wanasayansi wa San Jose, Carlifonia Marekani walitangaza rasmi juu ya mpango mpya wa utalii angani hii ni baada ya kuanza harakati za kutengeneza hoteli ya angani ambayo itakua ikipaa maili 200 toka usawa wa ardhi ya dunia, ikibeba watalii ambao watakua wakiangalia mandhari ya anga kwa kutazama sayari na maajabu mbalimbali ya angani, kwani hoteli hiyo ambayo ni ndege itakua na dirisha zinazoonesha vizuri mazingira ya nje.

Gharama ya  safari moja kwa mtalii inadaiwa kuwa takribani dola millioni 9.5 za kimarekani na safari imepangwa kuwa  mwaka 2022, ambapo orodha ya wasafiri itakusanywa miezi 7 kabla ya safari hiyo, lengo la utalii huo ikiwa ni kuonyesha watu safari za wana anga zinavokua na kuelimisha kuhusiana na tetesi za kuwepo kwa viumbe tofauti na viumbe wa dunia.





 
Atas