wengi tumetazama filamu iliyochezwa South Africa inayoitwa "sarafina" japo hatujui kiundani zaidi kuhusu maisha halisi ya waigizaji katika filamu hiyo, leo nitakupa stori kiufupi ya nyota mmoja katika filamu hiyo. Pichani hapo juu anaitwa Leleti khumalo ni moja kati ya waigizaji kwenye filamu ya sarafina, ambapo jina "Sarafina" ndio jina alilopewa Leleti Khumalo katika filamu hiyo ilioelezea hali halisi ya South africa ilipokuwa ikitawaliwa na makaburu.
Leleti Khumalo amezaliwa tarehe 30 mwezi wa tatu mwaka 1970, katika nchi ya South Africa ndani ya jiji la Durban sehemu panapoitwa KwaMashu, Leleti Khumalo japo akiwa mdogo alianza kujikita katika sanaa alikuwa ni miongoni wa wacheza ngoma wa kikudi kilichoitwa Amajika kilichoongozwa na Tu Nokwe. Mwaka 1985 akashiriki shindano lilioandaliwa na Mbogeni ngema aliyekuwa muongozaji katika filamu ya sarafina, shindano likiwa na nia madhubuti ya kutafuta waigizaji wa filamu ya "sarafina"
Filamu ya sarafina ilianza kuigizwa jukwaani (on stage) kama igizo tu, Leleti khumalo alijizolea umaarufu toka hapo ambapo aliweza kupata tuzo mbalimbali kama vile tuzo za TONY na NAACP za muigizaji bora wa kike wa jukwaani. Baadaye mwaka 1992 Leleti khumalo na waigizaji wengine kama Whoopi Golberg, Miriam Makeba na John Kani wakaigiza rasmi filamu ya "sarafina" ambayo ilipata umaarufu mkubwa Africa na dunia nzima.
