Ni takribani miaka mitatu sasa imepita tangu waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kuama CCM na kwenda CHADEMA na kuungwa mkono katika kugombea uraisi mwaka 2015 na vyama vya upizani UKAWA. Baada ya kushindwa uraisi ziliibuka tetesi kwamba Edward Lowassa atarudi CCM lakini hakurudi kwa wakati huo.
Marchi mosi,ijumaa, Ule msemo wa waswahili unaosema lisemwalo lipo kama halipo basi laja, umedhihirika jana ambapo Edward Lowassa alionekana katika kumbi za Lumumba jijini Dar es Salaam akipokelewa rasmi na mwenyekiti wa chama cha CCM mheshimiwa John Pombe Magufuli raisi wa Tanzania.
Je? Nini maoni yako kuhusiana na kurudi kwa Edward Lowassa katika chama chake cha zamani CCM?